MADAM RITA AKIKARIBISHWA KWENYE BANDA LA ZANTEL NA MKUU WA MASOKO BW. DEEPAK KUMAR GUPTA
SALAMA J AKIPIGA PICHA NA MSHABIKI WAKE
MASTER J AKIPIGA PICHA MBELE YA TANGAZO LAKE LA EPIQ MOTO.
leo kwenye banda la Zantel Saba
Saba ambapo Majaji wa EBSS walipata nafasi ya kutembelea kujionea maonyesho
yanayoendelea ikiwa ni pamoja na kukutana na waandishi wa habari kuelezea
waliyoshuhudia katika usaili wa mikoa mitatu waliyopitia ya Dodoma , Zanzibar
na Lindi . Pia waliweza kutoa sifa wanazoziangalia katika kutafuta vipaji vya
muziki pamoja na kueleza eneo la usahili unaofuata wiki hii plae mjini Arusha
sehemu inayoitwa Triple A.
Pamoja na hayo, Mkuu wa
Masoko kutoka Zantel bwana . Deepak K. Gupta na Mkuu wa mawasiliano Awaichi
Mawalla walipata nafasi ya kuelezea njia mpya ambayo wenye vipaji vya kuimba
lakini wakakosa nafasi ya kufanya usaili wanaweza kufanya usaili kupitia simu
zao za mkononi. Mfumo huu ni wa sauti ambapo mshiriki anapewa nafasi ya kuimba
nyimbo aitakayo kwa muda usiiozidi dakika moja na kuweza kupata nafasi ya
kusikilizwa na Majaji.